Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XKILIMO

KILIMO: Fahamu Njia Nzuri Ya Kuondoa Magadi(Salts) Shambani | Mshindo media.

NJIA NZURI ZA KUONDOA MAGADI(SALTS) SHAMBANI
https://www.kilimobiashara.org/
Utangulizi
Katika mashamba mengi tatizo la udongo na ardhi kwa ujumla kujaa chumvi au magadi limekuwa tatizo kubwa kwa wakulima wengi kwani magadi au chumvi huleta madhara makubwa sana kwa mazao na hata mazao mengine hufa kabisa pale
yanapooteshwa kwenye udongo wenye magadi mfano wa mashamba yalioadhirika ni Ndungu irrigation scheme, kitivo irrigation scheme, Dakawa, Kiroka na Mkindo irrigation scheme (Morogoro), Kinyasugwe scheme (Dodoma) pia baadhi ya maeneo ya Lower moshi,Mawala,Kikavu chini, na hivyo kufanya mashamba yalio na tatizo hilo yasitumike katika uzalishaji,makala hii itakusaidia kujua namna ya kurudisha ardhi ya shamba lako katika hali nzuri na kuzuia uwezekano wa magadi kuongezeka katika shamba lako na hii itaongeza uzalishaji kwani utaweza kuotesha mazao mengi na ya aina mbalimbali kama udongo wako utakuwa na hali nzuri ya kuupatia mmea wako maji na madini or (nutrients) za kuuwezesha kukua vizuri na kuzaa sana
AINA ZA MAGADI ZILIZOPO KWENYE UDONGO 
Kuna aina nyingi za chumvichumvi zilizopo ardhini na huwa katika viwango tofauti kulingana eneo moja na lingine na tofauti hii husababishwa na asili ya udongo wa mahali husika chumvi hizi ni kama Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi ya kawaida(NaCl), Potasium, Boron,Magnesium, Calcium, Phosphorous madini mengine ni muhimu katika ukuaji wa mmea lakini kwa kiwango kinachotakiwa na huwa ni sumu endapo yatazidi kiwango chake
NAMNA AMBAVYO MAGADI HUDHOOFISHA MIMEA
Madhara yatokanayo ma magadi ni makubwa sana na huleta hasara kwa wakulima wengi sana, kitaalamu magadi huzuia mizizi ya mimea kufyonza maji kwenye udongo na kuufanya mmea kushindwa kukua kwani maji ni muhimu katika mfumo wa mimea kujitengenezea chakula chake hata kama utamwagilia maji ya kutosha katika shamba lenye magadi bado mimea haitaweza kupata maji hayo (salts induce water stress to crops through matrix forces build up between the soil particles and the salts ion and hinder plant water uptake via capillarity and osmosis).
Pia magadi huharibu mfumo wa udongo(soil structure) na kuufanya udongo kuwa mgumu na kuzuia mizizi ya mmea kupenya vizuri kwenye ardhi na hivyo kupunguza udhabiti wa mimea iwapo shambani na kusababisha kuanguka angauka kwa mazao yanapofikia wakati wa kubeba matunda au maua kwani hukosa nguvu za kujishikilia kwenye ardhi na hali hii husababishwa sana uwepo na sodium nyingi shambani na mkulima hupata hasara kubwa sana.
VYANZO VYA MAGADI KWENYE UDONGO
Asili ya udongo wenyewe 
Baadhi ya maeneo yana udongo wenye asili ya chumvi kwa Tanzania maeneo hayo yanapatikana kwa wingi dodoma na singida na hasa wakati wa kiangazi baada ya mvua kukatika unaweza ukaona kabsa mabonge ya chumvi ardhini
Maji yanatumika kwa umwagiliaji 
Kuna baadhi ya maeneo maji yake huwa na chumvi kiasi  kwenye mito na hapa chemichemi na wakulima hutumia maji kutoka kwenye vyanzo hivyo vyenye maji ya chumvi katika kumwagilia mashammba yao, hii huongeza chumvi kidogo kidogo kwenye ardhi na kama mwendelezo wa kutumia maji hayo utafanyika kwa miaka mitano basi shamba hilo litakuwa limejaa chumvi na halitafaa tena kwa kilimo endapo njia na mbinu stahiki hazitachukuliwa
Utumiaji wa mbolea za viwandani bila maelekezo ya kitaalamu
Tujue ya kuwa sio kila mbolea ya kiwandani inafaa kwenye kila aina ya udongo, pili tunapokuwa tunaweka mbolea shambani lazima tuwatumie wataalamu ili watupe vipimo sahihi vya uwekaji wa mbolea hizi ili ziwe kwa kiwango kinachotakiwa pasipo kuzidisha wala kupunguza , kila shamba lina rutuba tofauti na lingine kwa hiyo ata uwekaji wa mbolea utatofautiana.
Pia kila zao lila vipimo vyake vya kiasi cha mbolea kinachotakiwa, kumbuka ni muhimu kufuata ushauri wa wataalamu kabla ya kuweka mbolea shambani ili kuondokana na matatizo na uweze kuzalisha mazao yenye tija ndio maana wataalamu kutoka MjasiriamaliPlus tunakushauri upime udongo kwanza kabla hujaanza kulima
Mfumo mbaya wa utoaji maji shambani(poor drainage system)
Tatizo hili ni kubwa sana hasa pale wakulima wengi wanapoamini kuwa katika kumwagilia shamba lazima aone maji yametuama ndio aridhike kuwa amemwagilia, hili ni kosa kubwa kwani tunatakiwa tujue kuwa mimea hufyonza maji yaliyo ardhini tuu(plants absorb water, and they don't drink water ......... Myth), maji yaliyotuama shambani hupandisha chumvi iliyopo chini kuja juu na baada ya ardhi kukauka chumvi ile hubakia juu ya ardhi na kuathiri mimea
NJIA ZA KUONDOA MAGADI SHAMBANI
Hili ndilo lengo kuu la makala hii ili kumsaidia mkulima kuondokana na tatizo hili, nitaeleza njia za kitaalumu na za gharama nafuu za kuondoa na kupunguza magadi shambani.
Kuzamisha chumvi(Leaching of salts)
Wakati wa kumwagilia shamba unashauriwa umwagilie maji mengi kiasi kuliko yale yanayotosheleza mmea wako ili maji hayo ya ziada yasaidia katika kuzamisha chumvi iliyoko juu wa udongo iende chini zaidi ambako mizizi ya mimea haifiki, njia hii lazima utumie wataalamu wa umwagiliaji (irrigation engineers) kama mimi ambao tutakusaidia kitaalamu kuendena na udongo wako na tutakuambia ni kiasi gani cha maji inatakiwa umwagilie katika shamba lako ili kuondoa chumvi na kusaidia mimea yako kukua (irrigation and leaching requirements)
2. Uwekaji wa Gypsum (Calcium Sulfate)
Gypsum hufanya kitu kinachoitwa neutralization ambapo hubadilisha chumvi iliyopo ardhini isilete madhara kwa mimea na katika maduka mengi ya pembejeo zinauzwa hizi gypsum kwa ajili ya mashamba ili kudhibiti chumvi na magadi lakini njia hii ni ya gharama kidogo
3. Utumiaji wa Samadi 
Mbolea za wanyama na mimea husaidia sana kwenye kuongeza rutuba kwenye ardhi pia katika kuhakikisha na kupungiuza magadi kwenye udongo na njia hii matokeo yake ni polepole lakini ina uhakika na pia samadi ina faida nyingine nyingi katika kuimarisha udongo na kuongeza upatikanaji wa madini kwa mimea
   4. Njia ya mafuriko (flooding)
Njia hii hufanywa katika maeneo yenye maji mengi na hasa kipindicha mvua , shamba lenye magadi hutifuliwa na kufurishwa au kumwagiliwa mpka maji yanatuama (wakati hamna mazao shambani) na baada ya hapo maji hutolewa kwa mifereji maalumu na maji hayo huchukua magadi katika shamba husika
NB. njia hii usiifanye kwenye mashamba yaliosongamana ili maji yaliyo na magadi yasiende kwenye shamba la jirani yako na kumpa hasara 
       5. Utumiaji wa njia za kisasa za kufanya umwagiliaji kama drip irrigation,sprinkler system hupunguza uwepo wa magadi kwenye udongo na kama unahitaji system hizi nitafute kwa mawasiliano mwishoni mwa makala hii
Lakini kwa maeneo ambayo yana magadi sana unashauriwa kupanda mazao yanayoshahimili ardhi yenye chumvi 
mazao yanayoshahimili chumvi zabibu, mbaazi, Nanasi, Miembe hasa mazao ya miti ndio hushauriwa sana katika ardhi yenye magadi 
mazao yasiostahimili udongo wenye magadi 
Mahindi,Tikiti maji,Nyanya, Mbogamboga, na mengne mengi.

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.