Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XBUSTANI

KILIMO BORA CHA MCHICHA I Mshindo media

Image result for mchichaKilimo cha mchicha ni rahisi kufanyika katika mazingira yote iwe ni katika bustani ya nyumbani au bustani ambayo si ya nyumbani, Mchicha unaweza limwa kwa lengo la kibiashara na kukidhi mahitaji ya nyumbani kwa lishe bora. Mchicha ni mboga za majani ambazo chanzo kizuri cha viini lishe, kuongeza damu katika mwili wa binadamu, vitamin C na madini.

Mchicha unahitaji maji ya kutosha katika kipindi chake chote cha ukuaji hadi kuvuna. Vilevile mchicha huitaji udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye kuhifadhi maji.

UTAHAYARISHAJI WA SHAMBA
Tengeneza shamba la mchicha kwa kutifua ardhi na kulainisha udongo wenye kina cha sentimeta thelathini. Weka mbolea ya samadi debe moja katika kila mita moja ya mraba. Panda mchicha katika matuta yenye upana wa sentimita tisini hadi mia moja (90SM kwa 100SM)

AINA ZA MBEGU
• Amaranthus hybridus huu ni mchicha wenye majani mekundu na mbegu zake ni nyeusi.

• Amarantus africana ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni ni nyeusi.
• Amaranthus hypochondriacus ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni njano hasa mbegu zake hutumika kutengeneza uji wa watoto wachanga.
• Amaranthus dubius ni mchicha wa kienyeji na Aspinosus ni mchicha wenye miba mingi.

UPANDAJI
• Changanya mbegu za mchicha na mchanga kwa uwiano wa 1:3, 1:4, 1:5 au 1:6 ili kurahisisha upandaji.
• Mchicha upandwe katika tuta kwa mistari yenye nafasi ya sentimita thelathini.
• Funika mbegu kwa kutumia udongo uliolaini na tandaza nyasi kavu baada ya kupanda ili kutunza unyevunyevu na toa matandazo baada ya siku tatu hadi tano tangu siku ya kupanda.
• Pandikiza mchicha kwa nafasi ya sentimeta kumi na tano kwa ishirini.
• Mwagilia maji ya kutosha.

KUKUZIA
Tumia mbolea ya samadi iliyolowekwa kwenye maji kwa muda wa masaa ishirini na nne kumwagilia mchicha wako ili kupata mavuno mengi zaidi. Tumia kiasi cha debe moja kwa kila mita moja ya mraba.

NAMNA YA KUDHIBITI WADUDU WAHARIBIFU
Adui mkubwa wa mchicha ni wadudu aina ya mafuta au kitaalamu zaidi huitwa APHIDS ambao hufyonza utomvu wa mchicha na kusababisha majani kujikunja, mchicha kusinyaa na kunyauka. Kudhibiti wadudu hawa mwagilia mchicha wako kutumia chombo kinachotoa maji mithili ya mvua kitaalamu kinaitwa “watering can” ili kuwadondosha wadudu hao.
Wadudu wengine ni kitambazi ambacho hula majani ndani kwa ndani hivyo tumia mwarobani kunyunyuzia majani ili kuwaua wadudu hao waharibifu.

MAVUNO
Mchicha huwa tayari kuvunwa baada ya majuma matatu hadi sita tangu kupandwa au kupandikizwa. Uvunaji huweza kuendelea kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu kutgemeana na namna utakavyoamua kuuvuna mchicha wako.

KIASI CHA MAVUNO
Kila mita moja ya mraba huzalisha kiasi cha kilo nne hadi tano za mchicha. Hii inamaanisha kuwa utapata kiasi cha tani ishirini hadi arobaini kwa hekta moja ya mchicha.

NAMNA YA KUHIFADHI MCHICHA KWA SIKU NYINGI ZAIDI
• Baada ya kuvuna funga mashina ya mchicha na weka kaatika chombo chenye maji kwa kufanya hivyo unaweza kuhifandhi mchicha kwa muda wa masaa ishirini na nne yani siku moja.
Ili kuhifadhi mchicha kwa zaidi ya miezi mine fanya kama ifuatavyo:-
• Vuna mchicha wako kisha usafishe vizuri
• Funga kaitika mafungu mafungu
• Chemsha maji mpaka yachemke
• Tumbukiza mafungu ya mchicha katika maji yanayochemka kwa muda wa dakika moja hadi mbili.
• Kausha vizuri chini ya kivuli na utunze mchicha wako katika sehemu isiyo na unyevunyevu.
.....................................................................................................

About Anonymous

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.