Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XBIASHARA

KILIMO CHA VITUNGUU SAUMU I Mshindo media
https://mjasiriamaliplus.blogspot.comBadili Maisha Yako Kwa Kuwekeza Kwenye Kilimo Cha Vitunguu Swaumu 


Mahitaji ya hali ya hewa na udongo 
Zao hili hupendelea hali ya hewa ya baridi na udongo tifu tifu na wenye rutuba. Sehemu 
nyingi zinazostawi vitunguu maji hufaa pia kwa zao hili. Maeneo ya mwinuko wa kiasi 
cha zaidi ya mita 1000 juu ya usawa wa bahari hufaa zaidi 

Maandalizi ya shamba 
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sen- 
timita 30 hadi 45 Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka kati kati ya 
tuta na tuta na upana wa mita 1 

Maandalizi ya Mbegu 
Kwanyua vipande/Vikonyo vya vitunguu sumu tayari kwa ajili ya kupanda katika nafasi. Mbegu sharti iwe imekaa kwa miezi mitano hadi sita tangu kuvuna ili iweze kuota. Ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri wa kitaalam ili kujua namna ya kutam- bua mbegu ya vitunguu saumu iliyo tayari kwa kupanda kwani ikipandwa kabla haijawa tayari haioti 

Upandikizaji 
Tumia mashine alama kuweka alama za kupandia katika nafasi ya sentimita 15 hadi sentimita 25 na mistari minne hadi sita kwa tuta Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda 

Palizi 
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. 

Mbolea 
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji. 

Matumizi ya viuatilifu 
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalam 

Mavuno 
Vitunguu saumu hukomaa miezi 6 tangu kupanda 

...............................................................................................................

    About Anonymous

    0 comments:

    Post a Comment

    Powered by Blogger.