Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XKILIMO

KILIMO BORA CHA PARACHICHI I Mshindo Media
Parachichi ni matunda ya bustanini na mashambani kwa wakulima wadogo.

Parachichi yana matumizi mengi yenye faida kubwa kwa wakulima na wadau wengine.

Matunda ni chakula chenye viini lishe bora kama Vitamini (A,B2, C, D,E,K )
na madini ( P,K, Mn, S ) ambavyo vinalinda mwili, mafuta kwa wingi ( 5-30%) ambayo huleta joto mwilini, protini (1-5%) ambayo hujenga mwili na kiasi cha calories 250 ambayo huleta nguvu mwilini.

Tofauti na matunda mengine,Parachichi ni malighafi ya viwandani kutengenezea madawa ya ngozi pamoja na vipodozi mfano mafuta ya nywele na ngozi,shampoo, sabuni na kadhalika.
Miti hutumika kama kuni, mbao nk.
Vilele majani yake na mbegu hutumika kama dawa.

Parachichi ni zao la chakula na biashara na huuzwa na wakulima na wafanya biashara wadogo na wakubwa kwa ajili ya kipato.

Aina za Parachichi Kuna aina nyingi za Parachichi zisizopungua 30 nyingi nzikiwa za kienyeji.

Hizi zimekuwepo katika mifumo yetu ya uzalishaji hasa katika nyanda za juu kusini na kasikazini kwa muda marefu, lakini uzaaji wake ni mdogo kutokna na ubora hafifu, kuzeeka na kuchakaa kwa miti na utunzaji hafifu.

Aina bora za mapararchici ambazo zimefanyiwa utafiti na kukubalika kwa wakulima na walaji ni pamoja na;

Aina hizi hutofautiana kwenye urefu wa mti, uzaaji wa matunda, ukubwa wa matunda, ladha na muda wa kukomaa.

Aina hizi zinazaa matunda mengi na bora pia huchukua muda fupu kukomaa.Kiasi cha matunda kwa mti kwa msimu ni kati ya 300 hadi 800 kutegemeana na matunzo.

Njia bora ya kuzalisha miche ya maparachichi kwa njia ya vikonyo Njia ya miche bora ni kutumia vikonyo. Faida zinazotokana na njia hii ni:

•Miti kuchukua muda mfupi kukomaa na kuzaa matunda (miaka 3-3 ½)
•Miti huwa na umbo na urefu wa wastani
•Kuzalisha miche yenye tabia moja. Mti haubadili tabia
•Kuepuka magonjwa hasa virusi
•Miche mingi kuzalishwa kwa wakati mmoja
•Kumwezesha mkulima kufanya uchaguzi

Hatua za kufuata kabla ya kuzalisha miche kwa njia ya vikonyo:

1.Kuzalisha miche ya kubebeshea vikonyo kutokana na mbegu
2.Kubebesha vikonyo kwenye miche

Vifaa vinavyohitajika:
•Viriba –mifuko ya plastiki yenye kipenyo cha 5’’-6’’ na urefu wa 5’’-6’’
•Udongo safi usio na magonjwa hasa wa msituni, samadi, mchanga/pumba za mchele kwa uwiano wa 3:1:1
•Mbolea ya TSP
•Mbegu za maparachichi

Njia;
1.Andaa kitalu sehemu wazi na tengeneza kichanja ili kuzuia jua na mvua.
2.Changanya udongo na jaza kwenye viriba
3.Panda mbegu kwenye viriba
4.Panga viriba kwenye kitalu
5.Mwagilia maji
6.Baada ya wiki 2-3mbegu zitaanza kuota
7.Tunza miche hadi kufikia umri wa kubebeshwa miezi 3-4 au unene wa pensile.

Ukuaji wa miche hutegemea hali ya hewa. Sehemu za joto mbegu huchipua upesi na miche kukua haraka.

Kubebesha vikonyo
Vifaa:
•Visu maalumu kwa ajili ya kubebeshea
•Jiwe la kunolea
•Mikanda ya nailoni (tapes)
•Mifuko ya nailoni kufunikia kikonyo
•Vikonyo Uchaguzi wa tawi kwa ajili ya vikonyo:
•Ni muhimu kuchagua tawi zuri kwenye mti uliokomaa na kuzaa matunda ili kuharakisha kukomaa na kuzaa kwa mti uliobebeshwa .
•Chagua kikonyo chaenye macho au vijichoza (buds) vyenye afya nzuri.
•Usichague kikonyo chenye maua
•Kikonyo kikianza kuchipua hakifai kwa kubebesha kwa sababu ni kichanga
Mambo muhimu katika ubebeshaji
•Miche inayobebeshwa itoke kwenye jamii moja, kwa mfano mparachichi na mparachichi, limau na limau au limau na chungwa nk.
•Urefu wa kikonyo uwe sm 15-20 na chonga kikonyo bapa sm 2- 3
•Mche wa kubebeshea kikonyo ukatwe juu kwenye shina sm 20-25 kutoka usawa wa udongo na kata kipenyo cha sm 2-3. Urefu wa kipenyo ulingane na urefu wa bapa la kikonyo
•Sehemu ya mmea yenye mirija ya kupitisha chakula na maji zihakikishwe zinaungana.
•Pachika kikonyo kwenye kipenyo cha shina na hakikisha kikonyo kina simama wima kwenye shina
•Fungia vizuri kikonyo kwenye shina na mkanda (strip) wa nailoni nyeupe. Tendo hili lifanyike kwenye mazingira safi na haraka ili utomvu kwenye bapa na kipenyo usikauke
•Funika mche na mfuka wa nailoni nyeupe yaani tube au rambo inayopitisha mwanga mradi isiwe nyeusi
•Tunza miche na hakikisha kuna unyevu wa kutosha kwenye mche na kitaluni ili miche ipone
•Hakikisha maji hayagusi ungio ili kuepuka maambukizi ya magonjwa
•Baada ya wiki 2-3 vikonyo vilivyopona vitaanza kuchipua
•Ondoa machpukizi/maotea yote yanayojitokeza chini ya ungio yaani kwenye shina la kibebesheo
•Majani yakijitokeza kwenye kikonyo ondoa mfuko uliofunika kikonyo
•Tunza miche kitaluni kwa kumwagilia maji na kuondoa machipukizi/maotea
•Baada ya miezi 3-4 miche itakuwa na majani 6-8 dalili ya kutosha kupandikizwa shambani

Utayarishaji wa shamba
•Chagua eneo la wazi lenye rutuba
•Eneo liwe na mteremko wa wastani ili maji yasituwame
•Eneo liwe jirani na chanzo cha maji
•Tayarisha shamba mapema kabla ya msimu wa mvua

Uchimbaji wa mashimo
•Pima nafasi za kupanda ambazo ni: 6m x 5m, 6m x 6m au 6m x 8m. Kwa nafasi hizi unaweza kuyarisha mashimo kati 220-400 kwa hekta
•Chimba mashimo kwa nafasi zilizopendekezwa. Urefu wa shimo sm 75 upana, sm 75 na kina sm 75
•Tenganisha udongo wa chini na wa juu
•Changanya udongo wa juu na samadi iliyooza kabisa debe moja
•Rudisha udongo wa juu kwenye shimo
•Weka kijiti katikati ya shimo
•Rudishia udongo wa chini
•Acha shimo kwa muda wa wiki 2 hadi mwezi 1 kabla ya kupanda

Kupanda
•Panda miche wakati wa masika
•Chimba kashimo kadogo katikati ya shimo kubwa ( palipo wekwa kijiti) waweza kuchanganya mbolea ya TSP gm 50 na CAN gm 50
•Chagua miche yenye afya nzuri
•Ondoa kiribu ( tumia kisu au wembe)
•Panda mche kwenye kishimo
•Sehemu iliyounganishwa isiguse udongo
•Shindilia vizuri na mwagilia maji ya kutosha

Utunzaji miche shamabani
•Fungua mikanda ya nailoni (tapes) iliyounganisha shina na kikonyo wiki 2-3 baada ya kupanda mche
•Shughuli nyingine muhimu ni palizi, kumwagilia maji, kuondoa machipukizi na kuzua magonjwa na wadudu

•Kupogole: ondoa matawi yanayogusa udongo
•Baada ya mwaka mmoja weka mbolea TSP gm 100 na CAN gm 100 kwa mche ili iweze kukua
 haraka na kuzaa matunda mapema.
...................................................................................................................................

About Anonymous

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.