Tikiti maji ni moja ya mmea wa matunda ambao umekuwa maarufu sana kipindi hiki, kibiashara na kwa matumizi ya chakula. Ni mmea huotao kwa kutambaa ardhini. Maua ya tikiti maji huchavushwa na wadudu hasa nyuki na huchukua takribani siku 65 mpaka 110 kutoka kusia mbegu mpaka kukomaa na hiyo hutegemea na aina, hali ya kimazingira/hewa na huduma.
Inastawi vizuri katika aina mbalimbali za udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kiwango cha uchachu kinahitajika ni 5.0-6.8 ili kuiwezesha mimea kufyonza madini vizuri.
Udongo wa kichanga mara nyingi huwa na uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na virutuisho vya mmea hivo umwagiliaji wa mara kwa mara na urutubishaji mzuri wapaswa kuzingatiwa ili kupata mavuno mazuri. Udongo wa mfinyanzi haupendekezwi sana lakini waweza leta mazao mazuri kama utamwagiliwa kwa umakini kuzuia maji yasituame hali inayoweza pelekea kutokeza kwa magonjwa.
Tikiti maji huathiriwa sana na hali ya joto ya chini sana au lililozidi sana. Tikiti hupendelea hali ya hewa yenye joto (18-350 C) na mwangaza wa jua wa kutosha. Kiwango kidogo cha unyevu kwa sababu unyevu mwingi unasababisha maradhi na huweza kuathiri utamu wa matunda
Nafasi na mahitaji ya mbegu

Ukubwa wa matunda unaohitajika ndio utakao eleza nafasi inayopaswa kuachwa katitati yamimea. Tikiti laweza pandwa kwa nafasi ya mita 0.6 mpaka mita 1 kutoka mmea mmoja kwenda mwingine na mita 0.9 mpaka mita 2 kutoka mstari moja kwenda mwingine Kwa wastani, ekari moja huhitaji kati ya gramu 400 mpaka gramu 700 kutegemea na nafasi ya kupanda itakayotumika.
Urefu wa shimo la kupandia mbegu ni kuanzia sm 2 hadi sm 4. Kutegemea na hali ya joto ya eneo husika tikiti maji huchipua kuanzia siku 5 mpaka 10
Muda mpaka kukomaa/kuvuna
Kwa mbegu nyingi za hybrids tikiti maji huchukua siku 60 mpaka siku 85 kutoka kupandwa hadi kukomaa kutegemeana na hali ya joto na huduma.
..........................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment