Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XBIASHARA

KIJUE ZAIDI KILIMO CHA TIKITI MAJI HATUA KWA HATUA I Mshindo Media

 SEHEMU YA TATU

MBOLEA

Unashauriwa kuupima kwanza udongo ili ujue kiwango cha madini yaliyopo na uchachu wa udongo kabla ya kuanza kupanda. Hii itakusaidia kujua aina na kiwango cha mbolea kihitajikacho kwa zao lako.

Lakini kulingana na watu wengi kutoweza kuifikia huduma ya upimaji wa udongo mfumo wa kawaida waweza tumiwa.

Mbolea ya kupandia

Waweza tumia mbolea za wanyama/mboji ingawa zinaweza kuwa na changamoto zake kama vile:

 • upatikanaji,
 • usafirishaji na
 • uhitaji wa nguvu kazi kubwa
 • kama mbolea haitakuwa umeoza vizuri yaweza kuwa na vimelea vya magonjwa.

 Kwa mbolea za viwandani waweza tumia molea yenye kiwango kikubwa cha madini ya fosiforasi (P) ili kuwezesha mimea yako kutengeneza mizizi ya kutosha na yenye nguvu.

 Mfano wa mbolea hizo ni TSP, DAP na NPK.

MBOLEA YA KUKUZIA

Washauriwa kutumia molea zenye kiwango kikubwa cha naitrojeni (N) ili kuufanya mmea kutengeneza majani ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha chakula.

Mfano wa mbolea hizo ni CANNPKCalcium nitrate nk. (Zingatia matumizi ya mbolea za nitrojeni yakizidi kwenye mimea ya matunda hupunguza uzaaji na ubora wa matunda hivo matumizi lazima yazingatie hali ya udongo husika)

Wakati wa kutoa maua, kutengeneza na kukomaa kwa matunda

Hatua hii utahitaji mbolea zinazosaidia kutengeneza/kuimarisha maua, kufanya tunda liwe na maji na sukari/tamu na linalohifadhika kwa muda mrefu.

Hivo basi madini ya Boroni (B), Calsium (Ca), na Potasiumu (K) ni muhimu sana. Hayo madini waweza yapata kwenye mbolea kama Calcium nitrate, NPK, MOP, mbolea mbalimbali za majani (boosters) nk. Hapa mkulima anaweza changanya mbolea kama NPK na calcium nitrate au na MOP.

SEHEMU YA NNE:UMWAGILIAJI

Mahitaji ya maji/umwagiliaji

Kwa matokeo mazuri tikiti maji huhitaji maji ya kutosha lakini yasiwe mengi kiasi cha kutuama  kwa muda mrefu. Umwagiliaji wapaswa kufanyika kutegemea na hali ya hewa kama vile jua na na hali ya joto  na uwezo wa udongo kuhifadhi maji.

Kwenye udongo wa kichanga umwagiliaji wapaswa kuwa wa mara kwa mara kutokana na uwezo mdogo wake wa kuhifadhi unyevu/maji, lakini udongo wa mfinyanzi umwagiliaji waweza fanyika kwa muda mrefu kidogo sababu ya uwezo wake wa kuhifadhi unyevu kwa muda mrefu kuliko udongo wa kichanga

Kinapofikia kipindi matunda yapo katika hatua za mwisho za kukomaa (kama wiki mbili za mwisho) anza kupunguza umwagiliaji wa mimea yako taratibu hii hufanya matunda yawe na sukari ya kutosha.

Kupunguza matawi

Mmea unapokuwa na matawi mengi, washauriwa upunguze baadhi ya matawi na kuacha matawi machache yenye afya. Punguza vitawi vidogo vinavyomea kutoka kwenye matawi makuu.

Uchavushaji

Uchavushaji ni muhimu sana katika uzalishaji wa zao la tikiti. Wadudu hasa nyuki ndio wakala mkubwa wa uchavushaji hivo basi mazingira yeyote hatarishi kwa wadudu hawa yapaswa kuzuiliwa.

Kwa mazingira ambayo nyuki ni wachache sana, weka mzinga wa nyuki ili kuhakikisha kuwa uchavushaji unafanyika. Maua ambayo hayajachavushwa ama uchavushaji hafifu hupelekea kudondoka ama kutengeneza matunda yenye maumbo mabaya.

Piga dawa za kuua wadudu wasumbufu wakati wa jioni hii itasaidia kuwakinga nyuki ambao huwa active sana alfajiri na kiasi fulani mchana.

Kupunguza  matunda

Ili kupata matunda yenye ukubwaa wa kutosha unapaswa kupunguza matunda katika kila mmea na kuyaacha 2 mpaka 4. Hii ni sababu ukiacha matunda mengi sana kwa mche mmoja utaambulia matunda madogodogo sana.

Ondoa matunda dhaifu pia ondoa matunda yenye maumo mabaya (deformed) na kuacha yale yenye umbo zuri bakiza matunda 2 au 3 kwa kila mmea kama soko lako linataka matunda makubwa au matunda 4 na kuendelea kama soko lako linahitaji matunda madogo madogo.

SEHEMU YA TANO:WADUDU

Tikiti maji kama yalivyo mazao mengine hushamuliwa na aina nyingi za wadudu kama vile aphids (wadudu mafuta), cutworms (sota), bollworms (viwavi), melon flies(nzi wa matikiti), vithripi (Thrips), minyoo fundo (Nematodes).

Wadudu mafuta (aphids)

Wadudu mafuta ni wadudu wadogo sana. Wakiwa wakuwa huwa na uwezo wa kuruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Wadudu hawa hushambulia kwa kufyonza majimaji ya mmea hali isababishayo kukauka kwa majani yaliyoathiriwa na hupatikana kwenye buds, shina na upande wa chini wa majani.

 Dalili

 • Majani yanajikunja kwa kuelekea chini.

Wadudu mafuta ni hatari kwa vile huhusika katika usambazaji wa vimelea vya magonjwa hasa virusi.

Udhibiti

Tumia dawa zilizosajiliwa na mamlaka husika kwa mfano imidaclopid, piricarb, dimethoate nk.

Kwa vile mara nyingi wadudu hawa huwa chini ya majani ambako huwa vigumu kufikiwa na sumu, hivo wapaswa kutumia sumu penyezi (systemic insecticides) ama kuhakikisha nozo za pampu yako zipo vizuri na upigaji utakaowafikia chini ya majani.

Thrips (vithiripi)

Wadudu hawa ni wadogo sana hata zaidi ya wadudu mafuta.

Udhibiti

Tumia dawa zilizosajiliwa na mamlaka husika kwa mfano zenye kiambato kam imidaclopid, fipronil, diazinon, dimethoate nk.

SEHEMU YA SITA

Sota (cutworms)

Wadudu hawa hujificha kwenye udongo wakati wa mchana na usiku hujitokeza na hukata shina la mimea michanga sehemu ya chini karibu na usawa wa ardhi ukiwa mchanga.

Udhibiti

Tumia dawa yenye kemikali kama imidaclopid, acephate, lambdacyhalothrin, cypermethrin nk. Kwa ufanisi zaidi piga dawa kuzunguka shina la mimea kwenye udongo (drench) wakati wa jioni maana wadudu hawa mchana hujificha ndani ya ardhi kutoka wakati wa jioni/usiku.

Nzi wa tikiti maji (melon flies)

Nzi jike hutaga mayai ndani ya tikiti maji ambapo hupelekea kuoza kwa tunda.

MAGUGU

Magugu huathiri mazao kwa namna mbalimbali kama vile:

 1. Kutunza vimelea vya magonjwa na wadudu.
 2. Hushindana na mmea zao kupata virutubisho, maji nafasi.

Wapaswa kuanza palizi muda mfupi tu baada ya majani kuanza kuota hii ni kwa sababu kadri unavochelewa ndivo gharama za palizi na madhara ya magugu kwenye zao lako huongezeka.

Pia waweza tumia matandazo (mulches) kwani mbali na kuzuia magugu hupunguza upotevu wa unyevu katika udongo, huoza na kuwa mbolea endapo utatumia matandazo ya mimea.

SEHEMU YA SABA:MAGONJWA

Tikiti maji huathiriwa na Vimelea vya magonjwa mbalimbali kama vile  Fusari(Fusarium), Downy mildew, Ubwiri Poda (Powdery mildew), Anthracnose, Fruit Blotch na Gummy Stem Blight.

Damping off complex:

Ugonjwa huu hupendelea hali ya unyevu unyevu na ubaridi.

Udhibiti

 • Usiruhusu shamba lako kutuamisha maji au unyevu ulozidi kiasi
 • Tumia dawa za kukinga na magonjwa ya fangasi kama vile dawa zenye mancozeb au chlorothalonil.

Fusarium rot & crown rot

Ugonjwa huu huonekana kwenye mmea mdogo. Majani hupauka na hunyauka. Uozo wa njano ama wekundu kwenye kitako cha shina, kunyauka kwa mmea na kuoza matunda pamoja na uotaji wa fangasi nyeupe ni sehemu ya dalili za ugonjwa.

Udhibiti

 • Tumia mbegu kinzani.
 • Panda mimea yako kwenye matuta

 Fusarium wilt:

Mwanzoni mwa ugonjwa huu majani ya zamani hunyauka na huwa na rangi ya unjano. Mara nyingi unyauko huonekana zaidi wakati wa mchana kukiwa na joto jingi lakini hali hujirudi kidogo wakati wa masaa ya ubaridi.

Udhibiti

 • Tumia mbegu kinzani 
 • Panda kwenye matuta                                                                                  SEHEMU YA PILI

  Powdery mildew

  Hutokeza mabaka madogo madogo ya mviringo yenye rangi nyeupe kwenye majani pamoja na shina. Dalili hizi hutokea kwanza upande wa chini wa majani na baadae husambaa pande zote.

  Majani yaliyoathiriwa taratibu hubadilika kuwa ya unjano, hudhurungi na huishia kuwa kama karatasi na mwisho hufa.

  Udhibiti

  • Tumia madawa ya Triazole

  Ubwiri unga (Downy mildew)

  Hupendelea hali ya unyevu mwingi kama vile kipindi cha mvua.

  Udhibiti

  • Zuia kwa chlorothalon au mancozeb. Tibu kwa sulfur ama copper, metalyxyl

  Gummy stem blight

  Huu ugonjwa huathiri sehemu zote za mmea zilizo juu ya ardhi kwenye hatua yeyote ya ukuaji wa mmea kuanzia kwe mche mpaka mmea mkubwa. Mche hufa haraka sana baada ya kuathiriwa.

  Udhibiti

  • Zuia kwa chlorothalonil au mancozeb

  Ugonjwa wa chule/Anthracnose

  Hutoa viduara vya hudhurungi ama vyeusi katika majani vikianzia karibu na vena za majani.

  Udhibiti

  Zuia kwa chlorothalonil au mancozeb

  Sudden wilt

  Huu hutokea mwishoni mwa msimu wakati kuna matunda ya kutosha. Mwanzoni mmea hunyauka wakati wa joto kali la mchana hata kama kwenye udongo kuna unyevu wa kutosha.

  Lakini mmea hujirudi katika hali ya kawaida wakati wa usiku,lakini hali hiyo  huendelea kwa muda mrefu mpaka hali inakuwa mbaya na mmea hauwezi kujirudi tena katika hali ya kawaida tena .

  Udhibiti

  Kwa sasa hakuna dawa maalumu ya kuudhibiti ugonjwa.

  Bacterial wilt

  Mmea wote ama majani hunyauka majani uanza kuonesha hali ya ukijani unaofifia. Ugonwa huu huenezwa n wadudu hasa beetle(kombamwiko).

  Udhibiti

  Ugonjwa huu hudhibitiwa kwa kupambana na wadudu waenezao vimelea vya ugonjwa huu.         .........................................................................................................................

About Anonymous

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.