Pakua App Yetu Playstore Bofya Hapa!

XKILIMO

KILIMO CHA TIKITIKI MAJI HAPA I Mshindo Media

 USTAWISHAJI WA TIKITIKI MAJI

USTAWISHAJI WA TIKITIKI MAJI

USTAWISHAJI WA TIKITIKI MAJI : Zao la tikiti maji (Watermelon) asili yake ni Afrika na kwa sasa zao hili linalimwa sana Afrika Magharibi na Mashariki, India, Indonesia na katika visiwa vya Caribbean. Aina za matikiti maji zinazofahamika ni Tomo Waston, Dixie Queen, Charleston Grey, Congo na Florida Giant.

 

USTAWISHAJI:

Zao hili hustawi toka usawa wa bahari hadi mita 1000. Huvumilia aina tofauti za hewa na huhitaji unyevu wa kutosha katika hatua za mwanzo mradi tu upungue kadri inavyokaribia kukomaa. Unyevunyevu ukizidi sana husababisha magonjwa na hupunguza kasi ya utoaji wa maua. Pia joto kali hudhuru matunda.

 

KUPANDA:

Mbegu hupandwa nyakati za mvua na matunda huvunwa nyakati za kiangazi. Hupendelea ardhi yenye rutuba, utifutifu na usiotuamisha maji. Mbolea ya takataka au samadi ndiyo ifaayo zaidi kwa sababu mbolea za chumvichumvi ni ghali mno kwa zao hili.

Mbegu hupandwa katika matuta au vilima vya udongo. Weka mbegu mbili au tatu katika kila shimo, baadaye ng’oa na kubakiza mche mmoja ulio na afya. Umbali kati ya mche na mche ni sentimita 180 kati ya mstari.

Ni muhimu kupalilia na kurudishia udongo kwenye mashina ya mimea. Nyakati za ukame, unyweshaji ni lazima. Pia inapendekezwa kutandaza nyasi kwa kuzungushia mashina kusudi kuzuia mizizi isidhuriwe na jua.

Katika hatua fulani ya kukua, inapendekezwa kubinya au kukata ncha za mimea jambo ambalo linasababisha kutoka kwa matawi mengi pembeni, ambayo hatimaye hubeba matunda.

Matunda huwa tayari kuvunwa baada ya majuma 12 hadi 15 tangu kupandwa. Matunda huliwa mabichi. Mbegu zilizokomaa huwa na mafuta na watu wengi huzikaanga na kuzitafuna.

 

MAGONJWA:

Magonjwa ya zao hili ni sawa na yale ambayo hushambulia matango, yaani Cucumber Mosaic, Bacteria Wilt, Downy Mildew na Powder mildew.

Ugonjwa wa Cucumber Mosaic husababisha na sumu ya virusi ambayo ni mbaya sana kwa zao hili. Hutoa madoa kwenye matawi na kufanya sura yake kuwa mbaya na wakati mwingine rangi ya matunda ya kijani kibichi hutoweka kabisa. Hali ikiwa mbaya zaidi mmea hugeuka njano, hudumaa na kushindwa kutoa matunda. Ugonjwa huu huenezwa na wadudu kama aphids na beetles. Njia za kukabiliana nao ni kufanya usafi wa bustani na kandoni mwake, kuangamiza wadudu wauenezao, kuharibu mimea iliyoshambuliwa na kupanda aina zinazovumilia ugonjwa huu

Downy Mildew ni ukungu ambao huharibu matikiti na hasa nyakati za mvua na joto la kadiri husababisha madoa membamba na meupe au njano kwenye majani na matokeo yake ni kutoa matunda machache na duni. Ugonjwa huu hutibiwa kwa kunyunyiza dawa ya Copper au Zineb kila baada ya siku 10 na vilevile chimbia chini masalio ya mmea yaliyopatwa ugonjwa huu.

Powder Mildew ni ukungu ambao hushambulia majani na mashina ya mmea. Kwanza hutokea madoa madogo na meupe kisha husambaa kwenye mmea wote. Hatimaye rangi ya majani hufifia na mmea kufa. Ugonjwa huu hutibiwa na unga wa salfa kila baada ya siku 10.

 

WADUDU:

Cucumber Beetle mdudu huyu hushambulia miche ya zao hili mara inapochipua pia hushambulia majani ya mimea michanga. Njia ya kukabiliana na mdudu huyu ni kutumia dawa kama Rotane na Crylite kwenye miche michanga na kurudia kila baada ya juma moja.

Melon Aphids – mdudu huyu hufyonza utomvu wa mimea na kushambulia sehemu za chini za majani ambayo baadaye hukunjana. Huweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa ya maji ya unga ya Malathion au Nicotine . Hakikisha dawa inafi ka upande wa chini wa majani.

Pickle Worm – hushambulia sana matikiti, buu au funza hujipenyeza ndani ya ua au kitumba cha mmea, mwishowe huhamia kwenye tunda, mafunza mengine hutoboa mashina na kuishi ndani yake, lakini madhara zaidi hufanywa kwenye tunda. Njia ya kukabiliana nao ni kukusanya na kuchoma mimea na masalio yote yaliyokwisha ambukizwa na kunyunyizia dawa ya Rotane na Crylite kila baada ya juma moja.

About Mshindo Media

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.